Soma hotuba kamili ya Dkt. Wilbroad Slaa

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari jana Serena Hotel jijini Dar es Salaam
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari jana Serena Hotel jijini Dar es Salaam
Dkt. Wilbroad Slaa: Watanzania wana kiu ya kujua kwanini amekuwa kimya kwa muda mrefu sasa licha ya harakati za kisiasa kuendelea.
Muda utakaotumika ni saa moja, hakuna muda mrefu sana.
Ameamua kufanya hayo kwa kuwa imefika mahali ukweli lazima usemwe na upotoshwaji ukomeshwa. Namna pekee ya kufanya hivyo ni kutoka hadharani na kuusema ukweli.
Sote tunafahamu kuwa hana tabia ya kuchenga mambo, mengi yamesemwa na watu tofauti, kwenye mitandao, magazeti na viongozi wake!
Hana ugomvi na kiongozi yoyote, kwa kuwa siasa sio ugomvi. Kama binadamu wa kawaida hana chuki wala hasira na binadamu mwingine yoyote!
Iwe wazi kuwa katika Taifa kuna misingi ambayo inaongoza taifa. Inapofika mahali taifa linaongozwa kwa msingi ya propaganda na upotoshwaji matokeo yake ni vurugu kubwa katika taifa. Yeye amekataa hayo yote!
Anasema kuwa YEYE hakuwa likizo kama inavyosemwa na viongozi wake! Atafafanua kwa kifupi!
Kilichotokea ni kuwa aliamua kuachana na siasa, tarehe 28 Julai 2015, majira ya saa tatu usiku, baada ya kuona yanayofanyika ndani ya chama chake hayamridhishi.
Mtangulizi wa shuguli ambaye anatoka kwenye kampuni ya mahusiano ya umma anamtambulisha Dr. Willibrod Slaa. Anasema kuwa kwa muda mrefu Slaa amekuwa alama ya harakati za ukombozi dhidi ya makucha ya mkoloni mweusi.
Anaongeza kuwa Dr. ataongea kwa muda kisha kuruhusu maswali kutoka kwa waandishi, anamkaribisha!
Kinachosemwa ni kuwa Dr. Slaa alishiriki tangu mwanzo kwenye mchakato. Anasema ni kweli alishirii kwenye majadiliano, akaweka msingi na msimamo wako. Kuna wakati wengi wanashinda kutokana na wingi wao, wewe unayeamini katika misingi inabidi uachie ngazi.
Azam TV wameanza matangazo kupitia kipindi chao cha KITUO CHAKO CHA UCHAGUZI, wako LIVE sasa… Bado uchambuzi wa safari ya Kisiasa ya Dr. Willibrod Slaa unaendelea.
Tumepelekwa moja kwa moja kutoka Hoteli ya Serena
Mtangulizi wa shuguli ambaye anatoka kwenye kampuni ya mahusiano ya umma anamtambulisha Dr. Willibrod Slaa.
Anasema kuwa kwa muda mrefu Slaa amekuwa alama ya harakati za ukombozi dhidi ya makucha ya mkoloni mweusi.
anaongeza kuwa Dr. ataongea kwa muda kisha kuruhusu maswali kutoka kwa waandishi, anamkaribisha!
==========================
Slaa: Watanzania wana kiu ya kujua kwanini amekuwa kimya kwa muda mrefu sasa licha ya harakati za kisiasa kuendelea.
Muda utakaotumika ni saa moja, hakuna muda mrefu sana.
Ameamua kufanya hayo kwa kuwa imefika mahali ukweli lazima usemwe na upotoshwaji ukomeshwa. Namna pekee ya kufanya hivyo ni kutoka hadharani na kuusema ukweli.
Sote tunafahamu kuwa hana tabia ya kuchenga mambo, mengi yamesemwa na watu tofauti, kwenye mitandao, magazeti na viongozi wake!
Hana ugomvi na kiongozi yoyote, kwa kuwa siasa sio ugomvi. Kama binadamu wa kawaida hana chuki wala hasira na binadamu mwingine yoyote!
Iwe wazi kuwa katika Taifa kuna misingi ambayo inaongoza taifa. Inapofika mahali taifa linaongozwa kwa msingi ya propaganda na upotoshwaji matokeo yake ni vurugu kubwa katika taifa. Yeye amekataa hayo yote!
Anasema kuwa YEYE hakuwa likizo kama inavyosemwa na viongozi wake! Atafafanua kwa kifupi!
Kilichotokea ni kuwa aliamua kuachana na siasa, tarehe 28 Julai 2015, majira ya saa tatu usiku, baada ya kuona yanayofanyika ndani ya chama chake hayamridhishi.
Kinachosemwa ni kuwa Dr. Slaa alishiriki tangu mwanzo kwenye mchakato. Anasema ni kweli alishirii kwenye majadiliano, akaweka msingi na msimamo wako. Kuna wakati wengi wanashinda kutokana na wingi wao, wewe unayeamini katika misingi inabidi uachie ngazi.
Baada ya Edward Lowassa kukatwa na CCM Dodoma, Mshenga wake alimpigia simu na kuuliza nini kifuate baada ya tukio la dodoma. Akamuambia wawasiliane na mwenyekiti Freeman Mbowe, Gwajima nae akafika kwenye kikao hicho.
Msimamo wa Slaa ni kuwa ni lazima kumsikiliza mtu kabla ya kuamua nini cha kufanya. chadema ni cham cha siasa na hakiwezi kumkataa mtu yeyote kujiunga na chama.
Wakaweka vijana kuchunguza nini wanataka hao wanaotaka kujiunga na chama!
Slaa akataka kwanza Lowassa atangaze kutoka kwenye chama chake alichopo, kisha atangaze anakwenda kwenye chama gani. Atumie nafasi hiyo ya mkutano huo ajisafishe na tuhuma zote ambazo amekuwa akituhumiwa na watu.
Chadema ni cham ambacho kwa muda mrefu kimejijenga kwa msingi, na ni lazima wapokee mtu ambaye hawezi kukichafua chama chao.
Lowassa hakutangaza kujitoa, wala kujisafisha hadi kwenye mkutano ambao uliandaliwa na chadema. Slaa hakuhudhuria ule mkutano.
Kwenye kila jambo kuna jambo la kuzingatia. Mtu anayejiunga popote anakuja kama mtaji au kama mzigo? Lowassa anakuja chadema kama asset au liability?
Ijulikane, suala sio urais! Mpaka siku hiyo Slaa hakuwa amechukua fomu ya Urais kwenye chama chake. Slaa hakuwa anamzuia Lowassa kugombea urais chadema. Alitaka mgombea mwenye sifa na uwezo wa kukitoa Chama cha Mapinduzi.
Hakutamka popote kuwa anataka kugombea, hata 2010 hakugombea, aliombwa kugombea! Urais wake binafsi hauwezi kuikomboa nchi bila mchango wa jamii nzima.
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Suala la adha Lowaasa ni msizo au mtaji halikujibiwa hadi siku ya mkutano tajwa. Wakataka kujua anapokuja anakuja na akina nani, ni wafuasi wa aina gani; vijana wa bodaboda, vijana wasio na ajira au watu waliosombwa tu, au wanakuja kwenye mapambano?
Jibu lilikuwa ni kuwa tungepata wabunge 50 na wenyeviti wa CCM mkoa wasiopungua 22, wenyeviti wa CCM wilaya 88. Slaa akakiri kuwa kama ni hivyo kutakuwa na tetemeko (la kisiasa).
Wakahitaji majina ya hao waliotajwa kwa kuwa walikuwa kwenye mchakato wa kupitisha majina kwenye chama. KAtibu mkuu makini huwezi kuchukuwa watu usiowajua. Hakuna jina nililopewa mpaka tarehe 25.
Tarehe 25 wakamfata na kumuambia aitishe Kamati Kuu ya chama. Akakubali lakini akatahadjharisha kuwa hajapata majina na hajapata jibu kuwa Lowassa ni asset au liability. Lakini akaitisha kikao kwa kuwa ni jukumu la kikatiba la katiba.
Mwenyekiti akapiga simu, anasikia kuwa hajaridhika. Tangu 2004 Slaa hajawahi kugombana na mwenyekiti wake, isingekuwa sawa kama wangetofautiana kwenye kikao rasmi.
Wakakutana na Mwenyekiti, Gwajima, Lissu na wakajadiliana mpaka saa 9 mchana. Maneno kuwa alikuwa anakubaliana na mpango huo tangu mwanzo SI KWELI!
Mkutano ukashindikana. Wdau wakasema waende nyumbani kwa Lowassa, Slaa akakataa wakaenda Kamati kuu.
Kikao kikafanyika hadi saa 12 jioni. Ikaundwa kamati ndogo ya kumshawishi Slaa. Akakataa!
Akaandika barua ya kujiuzulu kwa kamati, Prof. Safari akaichana barua yake. Akaandika barua nyingine kwa Makamu-Zanzibar, makamu akamuambia kuwa haya mambo yamepangwa, asijisumbue!
Wanasema siasa ni mchezo mchafu, yeye anaaamini kuwa siasa ni sayansi! Asubuhi ya kesho akaandika barua, wasichojua ni kuwa kujiuzulu hakuhitaji barua. Maneno yakazuka kuwa Slaa hajaandika barua!
Upotoshwaji ukaendelea kuwa Slaa atazungumza na waandishi wa habari, wengine wakasema amefungiwa, amefungiwa na mkewe na kadhalika! Ukweli ni kuwa alikuwa na Lissu, Gwajima na Mbowe tangu asubuhi.
Maamuzi aliyoyafanya yanatokana nadhamiri yake!
Josephine nae ni mwanaharakati, ana sababu ya kuwa na uchungu. Alipigwa mwaka 2011 wakati wengine walijificha! Propaganda hizo tumeshazisoea!
Kama kuna mwenye ushahidi wa propaganda hizi aje, audited report zipo! Josephine halipwi na chama! Watu wanasema kuwa Slaa analipwa mil. 7, yeye ameendelea kula mihogo na maharage kama walivyoahidi mwaka 2010.
Wana uchungu na harakati!
Kikubwa katika harakati ni credibilty, jina la chama kilichojengwa kwa muda mrefu kisichafuliwe kwa namna yoyote! Mwanasiasa yoyote hataki kuchaguliwa, na Slaa nae hataki kuchaguliwa!
Wanasema kuna maslahi mapana ya taifa, ni nani anayapima? Lazima kuwe na kipimo cha kuapima hayo maslahi badala ya kutegemea mtazamo wa mtu!
Anafafanua suala la liability sasa!
Wamekuwa waongo kwa kuwa hakuna kipengele hata kimoja cha madai ya Slaa kimetekelezwa. Alisema wabunge waje kabla ya kura ya maoni ya CCM, kuja baada ya hapo ni kutafuta kichaka cha kujificha!
Watanzania wameijenga Chadema kwa damu yao, rasilimali zao! Watu hawawezi kukimbilia kirahisi wakati sio wasafi, akiwemo Sumaye na wengine. Nani hajua kama Sumaye ni fisadi? Kwa muda mrefu Slaa haongei na Sumaye kwa kuwa alimtuhumu kwa ufisaidi.
Sumaye ni mtu ambaye wanahabari walidai kuwa Sumaye alisema kuwa atahama chama endapo Lowassa atateuliwa, leo akageuka!
Leo anamsafisha Lowaasa, dhambi haisafishwa kwa dhambi. Anakumbusha jina la Mr. Zero (jina la utani la Sumaye).
Chama kimepokea makapi, na katibu alitahadharisha kuwa chama hakipokei makapi! Hakuna ambaye alijitoa kwa hiari, wengi walikuja baada ya kukatwa. Wenyeviti wengi ni mzigo, akiwemo Msindai.
Anangoja ajibu amlipue hadharani kwa kuwa alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za serikali z mitaa.
Siku aliyoambiwa aitishe kamati kuu aliuliza majina, akaambiwa anakuja chizi! Chizi ni nani, hata nyie hamumjui! Anaitwa chizi kwa kuwa ni mwizi wa kura ndani ya CCM.
Kuna haja gani ya kushindana kama tunampango wa kuiba kura pia. Wakamtaja Guninita, nani asiyemjua udhaifu wake? Hawezi kuandika hata ukurasa mmoja wa ripoti, amehama vyama mara kadhaa!
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Viongozi wa Chadema wamepata kigugumizi, waseme nani ameongeza thamani kwenye chama?
Najua maneno ya kuwa ni lazima kuiondoa CCM kwanza hata ikibidi tuweke mkataba na shetani, mimi ni padre wa Kanisa Katoliki! Kuwaondoa CCM kwa namna yoyote hakuleti maendeleo. CCM itaondolewa kwa program siriaz, sio kutumia watu wale wale!
Lazima tujue nini kilifanya Watanzania waamini chadema, kwa kuwa waliamini wana misingi isiyoyumba na uadilifu. Leo tunasimamia uadilifu?
Wanasema mwenye ushahidi aende mahakamani. Kama tusingewatuhumu Mramba na Yona wasingefikishwa kizimbani. Chadema imefungwa mdomo kwa kisingizio cha ushahidi!
Ni bora kukaa kimya kuliko kupotosha. Anasema nukuu ya biblia kuhusu wapotoshaji!
Inapofika mahali unapoambiwa hakuna mwenye dhambi ni makosa, dhambi haisahihishwi kwa dhambi nyingine! CCM wamekuwa waoga, wamewalea watu hawa kwa muda mrefu!
Kwa Wafrika choo ni neno baya, kwa wazungu choo ni rest room! Choo cha Kitanzania huwezi kukihamisha ndani ya chumba cha kulala na ukakiita choo, huwezi kulala kwa kuwa kitanuka, tena zaidi!
Ufisadi ilikuwa ajenda iliyowapa umaarufu CHADEMA, leo wamewachukua. Waanweza kuwa na ujasiri wa kukemea ufisadi?
Mwaka 2008 Slaa alikuwa bungeni wakati wa sakata la Richmond, anafahamu kwa uzuri anachokimaanisha. Bahati mbaya waandishi hawasomi makaratasi, na wabunge wa CCM pia.
Lowassa hatuhumiwi kwa habari ya Richmond pekee!
Lowassa aliambiwa na Slaa aache kulalamika, atangaze uhalali au uharamu wa Richmond, anamtaka aseme hao ‘wakubwa’ ni akina nani? Ni afadhali sifa yake iharibike kuliko kusema uongo.
Ni aheri kupotea kwenye siasa za dunia kuliko kusimamia uongo!
Msingi wa kwanza wa Richmond: Ili uelewe ni lazima urudi kwenye taarifa ya Kamati ya Mwakyembe, Slaa alifuatwa asubuhi ya siku ile kupewa rushwa, anashuru Sitta na Mwakyembe wajitokeze!
Akamuuliza mtoa rushwa kama anatoa m.500 kwa mbunge, atakuwa nazo ngapi? Aliwaambia Sumaye na Lowassa kuwa rushwa ni jambo linaloanzia kifuani kwanza. Mwanzo wa jambo hili ni taarifa ya Baraza la Mawaziri la 10.2.2006. Kamati ya mwakyembe iliangalia faili la kikao kile kisha kuandika ripoti!
Suala hili lilianzia wakati wa utawala wa mkapa kutokana na dharura ya umeme nchini, wakawasiliana na kampuni moja ya Amerika Kaskazini kwa suluhu ya muda mfupi ya umeme.
Serikali ya Kikwete ikapokea lile suala. Wakaruhusu mpango uendelee, ila kwa kufuata sheria. Hiyo ilikuwa kauli ya Baraza la Mawaziri!
Wakati auala lile linaamuliwa, Lowassa alikuwa Waziri Mkuu! Na ndie mwenye mandate ya maamuzi ya Serikali, iweje leo akane kuhusika?
Taarifa ya Mwakyembe inapotoshwa! Taarifa ilitaka Waziri Mkuu ajipime, au bunge limjadili na kumchukulia hatua. Lowassa akakimbia kwa kuwa alijua Bunge lingemfukuza kazi!
Waliioomba tenda walikuwa 26, waliorudisha walikuwa 8. Kamati ya Tathmini ikaona hakuna anayefaa hata mmoja! Waziri Msabaha akaagiza taarifa ile ifutwe na tathmini ifanyike upya, mara ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya nne. Jeuri wa Msabaha ilitoka wapi?
Baraza likaamua baadaye tenda iliyopewa kwa kampuni ya kwanza ifutwe! Lowassa alishiriki!
TANESCO wakatoa ushauriwa wao, Mamlaka husika ikatafute internatonal tender ya kununua turbine!
Lowassa akaingilia mchakato dakika za mwisho, akamuagiza katibu muhtasi wake!
Kwanini Lowassa, kwa kuwa anagombea urais, rais asiyeaminika hawezi kuchaguliwa!
Lowassa alishawahi kumuita Slaa kuhusu habari ya Meremeta, na kumuambia kuwa taarifa yake inaiaibisha Serikali! Kampuni ya jeshi imewahi kutengeneza gari, imehujumiwa na wahuni. Akamtaka Lowassa amuambie ni nani aliyehusika?
Akamuita mwingine kwnye Speaker lounge. Slaa akamuambia kuwa yeye ni fisadi kichwani, rohoni mpaka…!
Tunamsifia Lowassa kuwa an=taleta maji wakti jimbo la Lowassa halina maji na ufisadi mkubwa umefanyika kwneye jimbo hilo. Mnazungumzia shule za kata wakati wakati hamjua zimeanza wapi?
Slaa anataja nafasi alizowahi kushika Afrika. Uamuzi wa kujenga shule za kata ulifikiwa mwaka 90 huko Thailand, mpango huo ukaitwa Education for All, sio MMES kama unavyoitwa leo!
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Anasoma barua ya Ibrahim Msabaha kwa Flugence Kazaura, mkurugenzi wa bodi wa TANESCO!
Mpango ulikuwa kuondoa suala la umeme mikononi mwa tanesko kwa kuwa imeshindwa kutekeleza. Ugomvi wake na Masha ni kwa kuwa Lowassa alimlaumu Masha kuingilia mchakato wa serikali, akawekewa kinasa sauti chumbani.
Waziri Mkuu haruhusiwi na sheria kuingilia mchakato wowote wa tenda.
Kwenye kampuni nane zilizowasilisha maombi ya zabuni, Richmond ni kampuni iliyokuwa mbovu. Ilikuwa ni kampuni ya steshenari, sio umeme!Wakadai wana ushirikiano na kampuni nyingine ya umeme, kampuni hiyo ikakataa kujihusisha na Richmond, wala kuzalisha na majenereta!
Bill Clinton aliwai kukutwa na kashfa, walitaka kumchukulia hatua si kwa sababu ya zinaa, bali kwa kuwa alifanya uongo! Kwa kuwa alidanganya umma! Hata sheria za Tanzania zinakataza kuongopa, hata kesi za uchaguzi za Slaa zimethibitisha hilo.
Lowassa anadai yeye alisimamisha tenda, Slaa anaonesha uthibitisho wa hilo kwa barua za Lowassa kwenda kwa Msabaha zinazokanusha hilo, ‘Anaisoma’! Waziri Mkuu aliharakisha mchakato wa tenda, tofauti na sheria ya PPRA. Barua imeandikwa miezi mitatu baada ya mkataba kusainiwa, kwa maagizo ya Waziri Mkuu.
Tanesko ikaagizwa kusaini mkataba ambao haikuhusika kwenye kuujadili! Anaona aishie hapo… Anaupigia chapuo mdahalo wa Sitta na Mwakyembe, anasema Lowaasa nae afike kuondoa utata na kusema ukweli!
Chadema ni chama kilichotoa matumaini kwa vijana wengi! Isifike mahali tukawa washabiki kama 2005 ambapo watu waliahidiwa maisha bora, wakajikaanga kutokana na ushabiki! Anatoa ushahidi wa kitakwimu wa mfumuko wa bei…
Slaa ana uchungu kuona chama alichokijenga, kikifikia hatua ya kusomba watu kwa mabasi na malori kisha mkasema mafuriko hayazuiliki! Hayuko tayari,… Anakataa kuwa ZEZETA!
Ajenda ya Chadema ni nini, ilikuwa ni rushwa! Wananchi waliamini kwa kuwa msingi huo ndio unakijenga chama!
Sehemu kubwa ya kilichosemwa Jangwani ni ilani ambayo ilishaandaliwa tayri, hakuna kipya kilichosemwa. Kinachomuuma ni chama makini kuwa kibovu zaidi ya Chama cha Mapinduzi!
Hatuwezi kujenga maadili tukiwa na watu wachafu, anaishi na mwanamke bila kufunga ndoa kwa kuwa Serikali ya CCM haitaki afunge ndoa. Kesi yake ililetwa na mawaziri, waandishi wa habari na mtu kutoka IKULU. Ndoa inafungwa na Mungu!
Scotland Yard iliamrisha Lowassa achunguzwe, inakuwaje leo tunamtetea? Huu ni ushabiki usio na vielelezo, Slaa ana ushahidi! Hakuna ulazima wa kwenda mahakamani kwa kuwa kesi ya rushwa ni jinai, ni kesi ya serikali! Slaa au mwingine hana locus ya kwenda mahakamani kwa kesi ya jinai!
Mwakyembe alisema kesi ya jinai haina mwisho (kama zilizyo za madai).
chadema iliahidi kusafisha nchi kwanza endapo itashika dola, huku maendeleo yakiendelea!
Anasoma barua ya mchakato wa Richmond kuwa DOWANS. Kampuni imesajiliwa Costa Rica, na mwenyekiti asiye na anuani, simu wala jengo! Siku iliyosajiliwa, mmiliki alisajili makampuni mengine 99! Zaidi ya hayo ana makampuni mengine zaidi ya 50, DOWANS ni jina tu. Kampuni haipo!
Dowans sio kampuni halisi huko Kosta Rika, nchi nzima hakuna kampuni yenye uwezo wa kuzalisha umeme kwa kiwango hicho!
Leo Lowaassa anatuambia tufunge mdomo, huu ni udikteta! Anakumbusha sakata lake na Waziri Marmo…
Mabilioni ya fedha yanalipwa kwa kampuni ambayo haipo! Tunapenda ushabiki… Acha sifa iharibike!
Anasema hataki kuingia kwenye mambo ya Babu Seya! Vyuo vikuu vinatumia kesi ya Babu Seya kama case study. Mtoto mdogo hawezi kutoa ushahidi mahakamani, haki inapuuzwa kwa kuwa mtoto hawezi kutoa ushahidi!
Kesi ya Ulawiti rais hana mamlaka nayo, anatoa wapi kiburi cha kusema kuwa atamtoa?
Aliyeagiza polisi kuingia na polisi kuingia na mbwa msikiti wa mwembechai ni Sumaye, akiwa waziri mkubwa. Leo hii ni mpiga kampeni wa Lowassa! Leo tunataka kura kwa namna yoyote!
Ni afadhali kutokuwa na rais wa aina ya mtu huyu! anayesaka kura kwa kusaka huruma za watu. Slaa hayuko tayari kuona hilo linatokea…
Anahitimisha kwa kusema hajagusa chochote kuhusu ilani wala mkakati!
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Kama taifa tuna kazi kubwa ya kuchambua vitu nje ya shamrashamra, maneno matamu! Tumeshaumwa na nyoka, tusilaghaiwe na maneno ya watu hawa tena!
Utendaji uliotukuka unapimwa kwa utafiti, sio kwa ukasuku na kunukuu maneno ya wanasiasa!
Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu, matatizo ya wakulima na wafugaji yalikuwepo, alifanya nini? Lowassa aliwahi kubadili mpaka wa Monduli na Karatu na kusababisha mgogoro!
Mkampenia wake, Sumaye alisababisha matatizo ya ardhi Mvomero, akipora ardhi ambayo ilitakiwa yajengwe makao makuu ya Mvomero! Mengine ya Sumaye ameyaweka kiporo, hisa zake za kampuni aziweke wazi kama Sekretarieti ya Maadili inavyotaka!
Kutotangaza mali kunatosha kumtoa mtu ubunge! Sembuse Urais?
============================== =========================
Ukweli huwa una tabia ya kuegemea upande, anasemea speculation kuwa ameisema chadema peke yake.
Anasema amestaafu siasa, hana chama lakini bado anabaki kuwa mtanzania, mtetezi wa wanyonge na atabaki hivyo! Ataendelea kuwatumikia watanzania kadiri ya Mungu alivyomjalia vipawa! Kama alivyoombwa kugombea urais 2010!
Anaweza kuwatumikia Watanzania bila kuwa na chama!
Anasema kuwa hajapata vitisho kama alivyopata kipindi hiki, inazidi hata wakati alipotangaza List of Shame. Rostam ndiye anafadhili kampeni za urais wa Lowassa! Anamnukuu vitisho vyake! anakiri kuwa maaskofu wamehongwa, Rostam akiwa anaona, m60-m300!
Anasema hatenda chama chochote, anasisitiza! Amejitoa rasmi siasa za vyama vya siasa… Ataendelea kuwa msimamiaji wa anachokiamini!
Anawataka watu aliowataja watoke hadharani, anatoa baraka za KIMUNGU kwa nchi na watu wake!
Chanzo: Choice
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks