Taasisi ya Twaweza imetoa utafiti wake wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao inasema kuwa imeufanya kutoka kwa wananchi wa mikoa yote ya Tanzania bara.
Utafiti huo unaonesha kuwa kama uchaguzi wa Udiwani ungefanyika mwaka 2014 asilimia 60 ya wananchi wangepigia kura CCM.
Lakini mwaka huu wa 2015 kwenye udiwani asilimia 60 CCM, CHADEMA 24% CUF 2% ACT 1% UKAWA 3%
Mwaka 2014 Kwenye ubunge CCM 47%, CHADEMA 23%, CUF 4%
Mwaka 2015 kwenye ubunge asilimia 60 wataipigia kura CCM, CHADEMA 26%
Kwenye urais mwaka 2014 asilimia 51 wangeipigia kura CCM na CHADEMA asilimia 23
Lakini mwaka huu wa 2015 kwenye urais CCM wanaweza kupata asilimia 66%, 22% CHADEMA, CUF – 1%
ACT wazalendo – 0%, UKAWA – 3%, vingine – 6%, Hakuna jibu 2%
Kama uchaguzi ungefanyika leo asilimia 65% walisema Magufuli, 25% walisema Lowassa.
Magufuli anapendwa zaidi vijijini na Lowassa vijijini japo kote Magufuli anaongoza, kadri watu wanavyokuwa wazee wanamchagua Magufuli na Lowassa kwa vijana zaidi.
Zaidi ya asilimia 60 ya wasiosoma wako kwa Magufuli, nusu ya wasomi wako kwa Magufuli.
Kwanini utampigia kura mgombea wako, kwa Magufuli ni kwa sababu ni mchapakazi karibu wote na kwa Lowassa asilimia kubwa sababu anaweza kuleta mabadiliko.
Swali langu kwako kama uchaguzi ungefanyika leo, ungempigia kura mgombea wa chama gani?
0 comments:
Post a Comment