Baraza la Mitihani Tanzania – NECTA kimetangaza matokeo ya mitihani
ya darasa la saba iliyofanyika Septemba 9 na 10 mwaka huu ambapo mikoa
ya kanda ya ziwa imefanya vizuri ikilinganishwa na mikoa mingine nchini.
Akitangaza matokeo hayo jijini DSM, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo
Dk. Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa 51,8034 kati ya 76,3602
wamefaulu sawa na asilimia 67.84, ambapo kati yao wasichana wamefaulu
kwa asilimia 64.60 na wavulana asilimia 71.58 huku kiwango hicho cha
kikiongezeka kwa asilimia 10.85 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana wa
asilimia 56.99.
Dk. Msonde amezitaja shule zilifanikiwa kuingia kumi bora kitaifa
mwaka huu ni pamoja na shule ya Waja Springs ya Geita iliyoshika nafasi
ya kwanza ikifuatiwa na Enyamai ya Mara na Twibhoki pia ya Mara katika
nafasi ya tatu huku zikifuatiwa na shule nyingine 7 zote kutoka mikoa ya
kanda ya ziwa. Shule ya Mwashigini ya mkoani shinyanga imetajwa kushika
nafasi ya mwisho.
Katika hatua nyingine Dk. Msonde amezungumzia pia kukamilika kwa
maandalizi ya mitihani ya kidato cha nne ambayo itafanyika kuanzia nov
mbili hadi 27 mwaka huu na kuwataka wasimamizi pamoja na watahiniwa
kujiepusha na vitendo vya udanganyifu ili kuepuka kufutiwa mitihani
hiyo.
Kwa kuwa mitihani hiyo inafanyika tanzania bara na visiwani Dk Msonde
amewatoa hofu watahiniwa wa Zanzibar ambako kuna hofu ya uvunjifu wa
amani kutokana na masuala ya kisiasa kuwa mitihani hiyo itaendelea kama
kawaida kwani suala la ulinzi limeimarishwa.
Tazama matokeo hayo hapa; http://www.wavuti.com/2015/10/matokeo-ya-mtihani-wa-kitaifa-wa-darasa.html
Chanzo: Wavuti
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment