MIDA YA WANGA 2

Nilifungua lile sufuria kwa mara  nyingine na kutoka na kipande cha mkono nikakitazama na kuachia tabasamu, tabasamu lililogeuka na kuwa kicheko.Kilikuwa kicheko cha fedheha kwani kovu lililokuwa kwenye ule mkono nlilikumbuka barabara na kukumbuka mazingira ambayo tulikuwa tumemtoa yule mtoto. Alikuwa kalala na mama yake aliyekuwa kamkumbatia sawasawa huku biblia ikiwa kando yao. Sikutaka kutunza kicheko nlichokuwa nacho,  nilijikuta naangua  kicheko kwa jinsi yule mama alivyokuwa mjinga na mchache wa imani akidhani kulala na biblia kungetufanya tusitimize tuliyoyakusudi. Maskini mama yule,  sijui atalia kilio gani siku ya msiba wa mwanaye ambaye sasa namla nyama. Japo kwa kiasi fulani namlaumu mama yule kwa kutomtunza mwanaye vizuri kiasi cha mtoto kubaki mifupa. Wakati nikikumbuka yote hayo nilishtuliwa na mguso wa baridi mgogoni. Niligeuza shingo taratibu na nilichokiona sikutaka kuamini.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks