Kwahiyo usiku wa leo tungependa kuona ukimtoa mamako kipenzi Zakish kwetu kama kafara kubwa ya kufunga mwaka huu. Na hutoishia kutoa tu kafara bali utatengeneza nyama yake kisha kutuhudumia. "Hamza alimaliza kuzungumza huku akionyesha tabasamu usoni mwake, tabasamu lililogeuka na kuwa kicheko.Kicheko cha dharau na fedheha kisha akanitizama, akanishika bega na kuondoka. Sikutaka kuamini niliyoyasikia, ghafla machozi yakaanza kunitiririka taratibu kwa mara ya kwanza, nikakumbuka ni miezi minne tangu kumtoa babangu na mwanangu kipenzi kafara, leo tena nimtoe mzazi pekee na ndugu niliyebaki naye, haitowezekana! kwanza sijaomba kupandishwa cheo na sitaki!
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment