Baada ya kuonana na Waziri Mkuu,Hili ndilo walilozungumza wafanyabiashara wa Tanzania



leo jumuiya hiyo ya wafanyabiashara hao wametoa tamko lao ambalo limesomwa na Makamu mwenyekiti wa Shirikisho hilo Mr. Patrick Masagati amesema>>’Ikumbukwe Wafanyabiashara walifunga maduka yao maeneo mbalimbali nchini tangu Jumatatu kufuatia Mamlaka ya Mapato Tanzania  Tanzania[Tra] kusambaza barua na notes za ununuzi wa mashine za kielektoniki za Efd ndani ya siku 14.

‘Hapo awali kulikua na makubaliano ya kuundwa kwa kikosi kazi kilichoahidiwa na Waziri wa Fedha Mh.Sada Mkuya lakini kabla ya kutekelezwa hayo Wafanyabiashara walisambaziwa barua hizo za Notes’
‘Ikumbukwe kabla ya wafanyabiashara kufunga maduka yao viongozi tulitumia njia mbalimbali za kuondoa hali hiyo ya mgomo bila mafanikio,hapo awali tuliandika barua ya kuomba kuonana na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’
‘Kufuatia kauli zinazopingana za Mawaziri wawili yaani ile ya Waziri wa Fedha na ile ya Waziri wa viwanda na Biashara 2Feb 2014 tuliwasirisha barua ya kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu na kumkabidhi ndg.Salver Rweyemamu’
‘Siku ya tarehe 11February 2014 tulienda kufatilia majibu ya barua hiyo na kupewa ahadi ya kukutana na Katibu wa Rais Bw.Prosper Mbena siku ya 12 February saa 3 asubuhi alihitaji kujua kero na malalamiko yetu ili aweze kumshauri mh.Rais ili aweze kukutana na sisi’
‘Tulifanikiwa kumueleza hoja zetu na kuahidi kuzifanyia kazi ili tuweze kukutana na Mh.Rais lakini siku hiyo hiyo tulipokea mualiko kutoka ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kwa Naibu Waziri wa Fedha kwa maagizo kwamba Waziri alikua anahitaji kuonana na sisi haraka na kutusikiliza’
‘Tulifarijika kusikia hayo na kufanikiwa kukutana na Mh.Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda,Waziri Mkuu alituomba kuelezea hoja na malalamiko yetu yaliyopelekea Wafanyabiashara kufunga maduka yao,tuliweza kumueleza kero mbalimbali na malalamiko mbalimbali’
‘Ifahamike hoja ya msingi ya malalamiko yetu yalikuwa ni ya kimfumo hali inayopelekea sintofahamu kubwa kwa wafanyabiashara katika kuendesha biashara zao,tuliweza kumueleza mianya mbalimbali ya rushwa iliyokithiri ndani ya bandari na jinsi ya matumizi ya EFD’
‘Mashine hizi za kielektoniki zinapelekea vishawishi vya rushwa kwa watendaji wa mamlaka ya mapato na mambo mbalimbali yanayowakabiri wafanyabiashara’.
Haya ndiyo makubaliano ya Wafanyabiashara na Waziri Mkuu.
1.Mh.Waziri Mkuu alitupongeza kwa jinsi tulivyoweza kutengeneza hoja ya kujenga na kuongeza mapato ya serikali na kubaini mianya mbalimbali ya rushwa na kuahidi kulifanyia kazi.
2.Mh.Waziri Mkuu kwa hatua za awali alizoweza kuzichukua ni kusitisha mgomo wa wafanyabiashara na kufuta barua za notes zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na utekelezaji wake usimamishwe.
3.Mh.Waziri Mkuu ameridhia kuunda chombo kitakachopitia mgumo mzima wa kodi nchini.
4.Mh.Waziri Mkuu ameahidi kuchukua hatua hatua stahiki baada ya kukutana na maofisa wa TRA.
5.Mh.Waziri Mkuu ameahidi kukutana na Waziri wa Fedha na kuona wanavyoweza kutatua tatizo hili kwa haraka. 


Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks