Wazazi wengi hawana habari kuhusu hatari zinazowakabili watoto wao wanapotumia vifaa vya tablets na simu za mkononi almaarufu kama smartphones.Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na BBC.
Takriban mmoja kati ya watoto watano walisema kwamba waliwahi kuona kitu kwenye vifaa hivyo ambacho kiliwafadhaisha kwa kiasi maradufu zaidi ya jinsi wazazi wao walivyodhania.ohusiana
Utafiti huo ulitumika ikiwa sehemu ya siku ya kuadhimisha Usalama wa Matumizi ya Mtandao.Utafiti mwingine umeonyesha kwamba wazazi wapatao zaidi ya 20% hawaangalii kwa karibu yale ambayo watoto wao hufanya kwenye mtandao.
Huku 90% ya wazazi waliohojiwa na BBC huko Uingereza wakisema kuwa wamewahi kuwatahadharisha watoto wao kuhusu usalama kwenye mtandao wanapotumia simu zao, wengi walisema kwamba wao huwaruhusu watoto wao kutumia vifaa hivyo bila usimamizi wowote.
Vizuizi vya wazazi
"Cha kusikitisha ni kwamba hamna yeyote kati yetu wa umri wowote ambaye hawezi kupata matatizo kwenye mtandao," alisema Tonny Neate ambaye ni mkuu wa shirika la Get Safe Online.
Bila kutumia vizuizi mbali mbali vya usalama na kibinafsi watoto huenda wakakumbana na mambo ambayo hayafai kwa umri wao ama umri wowote.
Bila kutumia vizuizi mbali mbali vya usalama na kibinafsi watoto huenda wakakumbana na mambo ambayo hayafai kwa umri wao ama umri wowote.
Usalama wa matumizi ya mtandao katika familia.
Utafiti huo pia ulionyesha kuwa watoto kati ya umri wa miaka 13-16 wamo katika hatari zaidi za ukatili kwenye mtandao wakilinganishwa na wale wa umri wa miaka 8-12. Hata hivyo wazazi hawana hofu ikiwa watoto wao waliozidi umri huo kutumia vifaa vya tablet.
David Emm,ambaye ni mtafiti wa usalama katika maabara ya Kaspersky alisema kwamba:
''siku hizi wazazi hawana habari kuhusu hatari za kutumia mtandao kwenye tablets na simu za mkononi kama walivyokuwa hapo awali mtoto alipotumia tarakilishi.
"Watoto wanapotumia rununu na vifaa vyake kuingia kwenye mtandao hutumia mtandao ule ule wenye hatari, alisema.
"Wengi wanadhani kwamba rununu na zile tablets hazihitaji kiwango sawa cha kinga kama tarakilishi. Lakini kadri asilimia kubwa ya wazazi ambao hawachunguzi kile ambacho watoto wao hufanya kwenye mtandao, mkondo huo wa mawazo unapaswa kugeuka."
Simu za kampuni ya Apple kama iPhone na tabiti za ipad tayari zina vizuizi ambavyo mzazi anaweza weka ili mtoto asiwezie kutumia.
Ni muhimu kuzifunga tandawazi kabisa au kutia umri mwafaka wa watu wanaoruhusiwa kutumia maudhui yaliyomo.
Kuna uwezekano wa kuwa na akaunti zenye vizuizi kwenye simu za Android na tablets.
Vidokezo kwa Wazazi.
Zaidi ya 50% ya wazazi walioshiriki utafiti huo wa BBC walikuwa wameweka vizuizi kwenye simu zao lakini 40% pekee ya wazazi hao walisema kuwa wamefanya hivyo kwenye simu za watoto wao pia.
Katika utafiti uliofanywa kwenye maabara ya Kaspersky, 18% a wazazi waliwahi poteza fedha au data kutoka kwa simu zao au tablets kwa sababu watoto wao walikuwa wakitumia vifaa vya wazazi bila ya kuandaliwa kwa karibu.
Watoto walio huru sana kutumia sana mtandao hununua programu za michezo kwenye internet au Apps, na hivyo kutumia pesa vibaya.
Kamapuni ya Apple hivi karibuni iliambiwa iwarejeshee wazazi kima cha dola milioni 32.5 ambao watoto wao walinunua programu hizo bila ya idhini ya wazazi.
Watu wazima pia wanaonywa kuhusu usalama wao kwenye mtandao wakati kampuni ya Microsoft ilipozindua utafiti wake wa kila mwaka kuhusu usalama wa watu kwenye mitandao.
0 comments:
Post a Comment