Hiki ndo kimetokea land +254:Magari ya umma yavuruga shughuli Nairobi


Huduma za usafiri jijini Nairobi zimekwama kufuatia hatua za wenye magari kugoma hii leo wakilalamikia nyongeza ya ada ya kuegesha magari jijini humo.
Maelfu ya wafanyakazi wamelazimika kutembea kwa miguu na wasafiri wa kutoka jijini kwenda maeneo ya mashambani nao kulazimika kuahirisha safari zao.
Mwenyekiti wa wenye matatu katika eneo la Mlima Kenya, Bwana Michael Kariuki, ambaye aliongea na chanzo chetu akiwa nje ya lango la kuingia kwenye afisi ya Gavana wa Kaunti ya Nairobi, alisema mzozo uliopo ni mdogo na waweza kusuluhishwa haraka..............................>>



"Juzi tulikuwa na Gavana Evans Kidero na tukakubaliana kiasi tunachopaswa kulipa lakini jana tulipofika wafanyakazi wa kaunti wakakataa kiasi tulichokuwa nacho," Bwana Kariuki alisema.
Jiji la Nairobi ni mojawapo wa kaunti ambazo zimebuniwa chini ya Katiba iliyopitishwa na wapiga kura na kuidhinishwa mwaka 2010 katika hatua ya kuimarisha huduma kwa wananchi.
Kaunti hizo mpya hata hivyo zimejikuta njia panda baada ya kupata madaraka bila fedha za kuandamana nayo; ambapo zimelazimika kuongeza kodi kama njia mojawapo ya kujiimarisha kiuchumi.
Mkuu wa polisi nchini Kenya, David Kimaiya aliagiza idara ya trafiki nchini Kenya kunasa magari yote yaliyofunga barabara za mji.


Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks