Singapore umetajwa kuwa mji ghali zaidi duniani kuishi kwa mwaka 2014 na kuipiku miji mingine 131 kwa mujibu wa taarifa ya Economist Intelligence Unit (EIU).
Nguvu ya sarafu ya mji huo ikiwa ni pamoja na gharama kubwa ya uendeshaji magari na kuongezeka kwa malipo ya huduma za umma kumechangia Singapore kuwa juu ya miji yote duniani kwa ughali wa maisha......................>>
Pia ni mahali ambapo nguo zinauzwa kwa bei ya juu kabisa kuliko miji yote duniani.
Singapore imechukua nafasi ya mji wa Tokyo, amao ulikuwa unaongoza kwa ughali wa maisha mwaka 2013.
Miji mingine mitano inayoongoza kwa gharama kubwa za maisha duniani ni pamoja na Paris, Oslo, Zurich na Sydney, huku Tokyo ukiporomoka hadi nafasi ya sita.
Mji wa New York unatumiwa kama kigezo cha utafiti wa shirika la EIU kuhusu gharama za maisha katika miji mbalimbali duniani. Wanaangalia zaidi ya bei binafsi 400.
0 comments:
Post a Comment