Beyonce alikava jarida la Time lililowataja watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani kitu ambacho kimeiongeza CV yake kwa kiasi kikubwa.
Mwimbaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja alizungumza katika video iliyowekwa katika mtandao wa jarida la Time na kuelezea hisia zake.
“Najisikia kama mama na mtoto wangu amekuwa mwenye ushawishi zaidi kwenye maisha yangu na kuwa mama, na kumwangalia mwanangu katika macho yake, imenifanya kuwa mwanamke na imenifanya kuwa imara sana.” Amesema Beyonce...>>>
Hii haikuwa kitu kidogo kwa Beyonce kwa kuwa ametimiza moja kati ya malengo aliyokuwa nayo katika maisha yake.
“Kupiga picha kwa ajili ya jarida la Time ilikuwa moja kati ya malengo yangu katika maisha. Ni kitu fulani muhimu sana kwangu kama msanii kwa sababu sio tu kuhusu mitindo au uzuri, ni kuhusu ushawishi niliokuwa nao katika utamaduni na kuwa kati ya watu wengine wenye ushawishi ni heshima kubwa kwangu.” Aliongeza.
Aliopoulizwa angefanya nini endapo asingekuwa na uoga alijibu:
“Niangalie. Nakaribia kukifanya. Na wewe unaweza kufanya pia.”
Wengine waliotajwa kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani ni pamoja na Pharrell Williams, Miley Cyrus, Barack Obama, Selena Williams na Kerry Washington.

0 comments:
Post a Comment