Ndege ya Delta Airlines aina ya Boeing 767-300 ilikua ikipaa urefu wa futi 38,000 angani na kisha ghafla rubani akawasiliana na abiria ili kuwajulisha kwamba ndege itatua kwa dharura Albuquerque ikitoka Atlanta kuelekea Los Angeles Marekani...>>>
Mmoja kati ya abiria wa ndege hiyo Jennifer Squires amesema “nilidhani kuna mtu ameumwa lakini baada ya muda kidogo rubani alisema sababu ni msukumo wa upepo kusababishia kioo cha mbele ya ndege kuvunjika kwa nje bila kuvunjika kwa ndani’
“Niliposhuka kwenye ndege niliomba kuona sehemu iliyovunjika na kupiga picha hii, nashukuru rubani kwa kutushusha salama na kuweza kutoa habari hii kwa wananchi wengine pia ndege nyingine iliagiziwa kuja kutufata kutoka Los Angeles” – Jennifer
0 comments:
Post a Comment