Dunia yote inaangalia kombe la dunia hivi sasa na Rihanna ni mmojawapo, hata hivyo mwimbaji huyo haangalii tu magoli bali hudeal pia na muonekano wa kila anayeugusa mpira....>>>>
Katika kupepesa macho yake wakati wa mechi kati ya Marekani na Ghana, Rihanna amejikuta akidata kwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ghana, Kevin Prince Boateng.
Kupitia Twitter Rihanna aliiambia dunia alichonacho, kimpira anaishabikia USA ila kwenye hili alihamia Ghana.
Kwa bahati mbaya mchezaji huyo ana mke na hivi karibuni amepata mtoto wa kiume.
Hapo mwanzo Rihanna alionesha kumzimia Ronaldo kwa hiyo hivi sasa Mghana amempiga kanzu.


0 comments:
Post a Comment