Producer ambaye pia ni rapper ambaye anaibadilisha rekodi ya Forbes na kuwa mwana hip hop wa kwanza kuwa billionaire baada ya kufunga mkataba na kampuni Apple, Dr Dre ameendelea kuonesha jeuri ya pesa alizonazo kwa kuwapa neema wengine pia pale anapokula bata.>>>>>
Dre anaripotiwa kuhudhuria katika bar moja inayoitwa Skybar alhamisi iliyopita, na kwa mujibu wa ripota wa mtandao mmoja wa Marekani aliamuachia mhudumu tip ya $5,000 ambayo ni zaidi ya shilingi za kitanzania 8,442,500.
Inaelezwa kuwa baada ya kumpa neema hiyo, Dre aliendelea kula bata na alihamia club nyingine ambako haikufahamika aliacha kiasi gani kingine cha pesa.
Hivi karibuni Dr Dre ameutambulisha mjengo mpya wa kifahari aliuonunua kwa dola za Marekani zaidi ya milioni 35.
0 comments:
Post a Comment