Vermaelen akubali kujiunga Manchester United msimu huu

Majeraha ya mara kwa mara yamemfanya Vermaelen ashindwe kuwa na maendeleo Arsenal na hivyo kumfanya akatafute bahati kwenye timu nyingine ambayo huenda ikawa ni Manchester United.
Majeraha ya mara kwa mara yamemfanya Vermaelen ashindwe kuwa na maendeleo Arsenal na hivyo kumfanya akatafute bahati kwenye timu nyingine ambayo huenda ikawa ni Manchester United....>>>>
Nahodha wa Arsenal Thomas Vermaelen amekubali dau la kujiunga na Manchester United msimu huu wa jua.
United lazima wakubali ada ya Arsenal baada ya Kombe la Dunia, ila Vermaelen ana matumaini ya kuhamia Old Trafford na anajiandaa kuondoka Emirates.
Mlinzi huyo wa kati Varmaelen ana mwaka mmoja pekee uliobaki kwenye mkataba wake Arsenal na amejiona mwenyewe akitolewa kwenye kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger anayewapanga Laurent Koscielny na Per Mertesacker.
Kocha mpya wa United Louis van Gaal ana hasira ya kuiimaarisha safu ya ulinzi ya United na anaamini Vermaelen anaweza kufanya vizuri akiwa naye.
Vermaelen, 28, amekuwa Arsenal kwa miaka mitano baada kusaini akitokea klabu ya Uholanzi ya Ajax. Alianza vizuri akiwa na Washika bunduki, ila majeraha yakazuia maendeleo yake.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks