
Baada ya rekodi ya uhamisho wa £65milion kutoka Liverpool kwenda Barcelona mshambuliaji Luis Suarez ameingia rasmi kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa kwa pesa ndefu zaidi...>>
Usajili wa Luis Suarez umeigharimu FC Barcelona kiasi cha £65milion na hii ni mara ya kwanza kwa Liverpool kuuza mchezaji kwa pesa nyingi hivi na ameingia kwenye orodha yenye wachezaji kama Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Neymar wa Brazil.
Suarez hataweza kuichezea Barcelona mpaka atakapo maliza adhabu yake ambayo amefungiwa mechi 8 za kimataifa na kutojihusisha na soka kwa miezi minne.

0 comments:
Post a Comment