
Nicolas Mgaya Katibu Mkuu Tucta akieleza juu ya makubaliano yaliyofikiwa kwenye baraza la pekee la katiba kwa wafanyakazi wote nchini.
Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA) kupitia Baraza la Pekee la wafanyakazi wote hapa nchini, wameazimia kuwa wao wanataka serikali moja tu ambayo ipo kwa sasa...>>>
Akizungumza katika mahojiano maalumu ya Taarifanews.com Katibu Mkuu Nicolaus Mgaya alifafanua kuwa, baraza hilo lilikaa na kutoa mapendekezo hayo kuwa wao wanataka serikali moja na sio vinginevyo, sasa kama mwakilishi wao akisema vinginevyo hayo sio makubaliano waliyokubaliana kwenye baraza hilo.
Mgaya alisema kuwa ana imani na bunge hilo maalum la katiba kwamba likianza kwa awamu ya pili watakuwa wamejifunza mengi na watafuata kile ambacho wananchi wamewatuma, na sio malumbano ambayo hayana tija na maana kwa Watanzania ambao wengi wao ni walalahoi.
Aidha aliongeza kuwa Wabunge hao wanatakiwa kuachana na maslahi ya vyama vyao, kwani wananchi wanataka katiba sio malumbano na maslahi ya vyama vyao ambavyo hakuna chama kwa sasa kina wanachama wapatao milioni 45, ila Tanzania ndio ina wananchi wapatao milioni 45, ambao wanakiu ya kupata katiba mpya yenye tija na kuleta maendeleo.
0 comments:
Post a Comment