Tathmini ya kina kati ya Man U vs Swansea City leo

Muonekano wa vikosi vya kwanza vya klabu za Man-Utd na Swansea City.
Muonekano wa vikosi vya kwanza vya klabu za Man-Utd na Swansea City.
Katika kuelekea mechi za ufunguzi wa Ligi Kuu nchini Uingereza leo tutaviangalia vikosi vya Manchester United pamoja na Swansea ambavyo vitakutana katika dimba la Old Traford...>>>

Mpaka sasa klabu ya Swansea city imekamilisha usajili wa aliyekuwa kipa namba mbili wa ‘The Gunners’ Lukas Fabianski pamoja na kiungo aliyekuwa akiichezea klabu ya Tottenham , Gylfi Sigurdsson 24.
Wachezaji walioondoka katika klabu hiyo mpaka sasa ni ‘Striker’ Mhispania Micho aliyeelekea katika klabu ya Napoli ya kwa mkopo.
Mwingine ni kiungo aliyeng’ara katika michuano iliyopita ya kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Uholanzi Jonathani de Guzman aliyekamilisa usajili wa kudumu na klabu ya QPR.
Kikosi hicho kipo chini ya Kocha Garry Monk na kinategemea zaidi ubunifu wa mastaa kama kiungo Jonjo Shelvey na mastraika wakali kama Wilfred Bony na Nathan Dyer.
Kwaupande wa Man-U, Van Gaal amekuja na mfumo mpya wa 3-5-2 ambao katika practical ama kiuhalisia uwanjani ni 3-4-1-2 ambapo fainal third itaunganishwa na kiungo Juan Mata atakaye sambaza mipira na pasi za mwisho kwa mastraika wa United ambao ni Rooney naVan Persie.
Mfumo huo unaonekana kukisaidia kikosi cha Van Gaal ambacho msimu uliyopita walimaliza ligi katika nafasi ya saba kwa kutumia mfumo wa 4-4-2 chini ya Kocha David Moyes.
Mpaka sasa Man-U imewasajili Ander Herrera, Luke Shaw na Vanja Milinkovic na walioondoka mpaka sasa Patrice Evra, Rio Ferdnand, Federico Maceda, Bebe, Alexander Buttner, na Vidic.
Katika mechi hiyo ya ufunguzi itakayo pingwa majira ya saa nane na dakika 45 mchana kwa saa za Afrika mashariki, Kikosi cha Van Gaal kinapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.
Kutokana hari na mzuka mpya uliopo kwenye kikosi hicho kwasasa huku uwongozi mpya wa kocha Van Gaal ukiwa kama ndio chachu ya kujiamini na pia ushindi wa mechi zao za kujipima ubavu dhidi ya klabu kubwa kama Real Madrid, Liverpool na Valencia.
Zifuatazo ni rekodi za klabu hizi mbili zilivyokutana kwa mara ya mwisho;
England – Premier League ‎(EPL)‎
Jan 11, 2014 Man Utd. 2 – Swansea 0
England – FA Cup ‎(FA)‎
Jan 5, 2014 Man Utd. 1 – Swansea 2
England – Premier League ‎(EPL)‎
Aug 17, 2013 Swansea 1 – Man Utd. 4
England – Premier League ‎(EPL)‎
May 12, 2013 Man Utd. 2 – Swansea 1
England – Premier League ‎(EPL)‎
Dec 23, 2012 Swansea 1 – Man Utd. 1
Mechi tano za mwisho walizocheza Man-U;
Aug 12, 2014 Man Utd. 2 – Valencia CF 1 FR
Aug 5, 2014 Liverpool 1 – Man Utd. 3 ICC
Aug 2, 2014 Man Utd. 3 – Real Madrid CF 1 ICC
Jul 30, 2014 Man Utd. 0 – FC Internazionale 0 ICC
Jul 26, 2014 Man Utd. 3 – Roma 2 ICC
Mechi tano za mwisho walizocheza Swansea;
May 11, 2014 Sunderland 1 – Swansea 3 EPL
May 3, 2014 Swansea 0 – Southampton 1 EPL
Apr 26, 2014 Swansea 4 – Aston Villa 1 EPL
Apr 19, 2014 Newcastle 1 – Swansea 2 EPL
Apr 13, 2014 Swansea 0 – Chelsea FC 1 EPL
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks