Wenger ailalamikia ratiba ya ligi


Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Ligi Kuu ingepaswa kuanza wiki moja baadae ili kuwapa wachezaji nafasi ya kujiandaa vizuri kutoka Kombe la Dunia...>>

Washika bunduki walikuwa na wachezaji 11 nchini Brazil, na mabingwa wa Kombe la Dunia Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lucas Podolski ndio waliorejea mpaka sasa..
“Tungeweza kumalizana na hilo wiki moja badae kwenye mashindano yote,” alisema Wenger.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anasema ameshindwa kukiimarisha kikosi chake baada ya kumalizwa nguvu Kombe la Dunia.
Ozil, Mertesacker na Podolski hawatocheza kwenye mechi ya ufunguzi ya leo ya Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace au mechi ya Ligi ya Mabingwa ya kwanza ya kumtafuta bingwa dhidi ya Besiktas.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa ni Juni 6, 2015 mjini Berlin na Wenger angependa kuona Uingereza inazifuata Hispania na Italy kwenye mechi za ufunguzi
“Kama huwapi wachezaji muda wa kutosha wa kupumzika au muda wa kujiandaa na kuwachezesha moja kwa moja, watapata majeraha,” aliongea Wenger.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks