Watu nchini Scotland wameanza kupiga kura itakayoamua nchi hiyo kuendelea kubaki katika Umoja wa Kifalme (UK) au kuwa taifa huru...>>>>
Wapiga kura watajibu “Ndio” au “Hapana” kwenye mapendekezo yenye swali: “Je, Scotland inapaswa kuwa taifa huru?”
Watu 4,285,323, asilimia 97 ya wapigakura waliosajiliwa, ikiwa ni idadi kubwa ya watu kujitokeza katika historia.
Kura zitapigwa kwenye vituo 2,608 katika nchi nzima mpaka saa 4 usiku. Matokeo yanatarajiwa mapema kesho Ijumaa asubuhi.
Karatasi za kura zitahesabiwa kwenye maeneo 32 ya nchini Scotland.
0 comments:
Post a Comment