Kocha Jose Mourinho amedai Diego Costa hataweza kucheza mechi tatu kwa wiki kwa sababu ya majeruhi ya sehemu ya goti aliyoyapata kwenye mechi alipokuwa na Hispania.>>>>>
Costa, ambaye amefunga mara saba kwenye mechi nne za Chelsea, alilazimishwa kukaa benchi kutokana na tatizo hilo ambapo timu yake ilitoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Schalke kwenye Ligi ya Mabingwa.
Japokuwa Mourinho hakwenda mbali na kuikosoa timu ya taifa ya Hispania kwa suala hilo, ila amedai kuwa wanapaswa kumtibu kwa uangalifu.
0 comments:
Post a Comment