Mshikiliaji wa Ballon d’Or amehusishwa na taarifa za kurudi Manchester United na kutaka kukiacha kikosi cha Carlo Ancelotti msimu ujao...>>>
Inaaminika kwamba United wametenga kiasi cha pauni milioni 60 ili kuweza kumrudisha Ronaldo England, naye Louis van Gaal yuko tayari kumpa mkataba mnono na kiasi cha mshahara wa pauni 290,000 kwa wiki.
Hata hivyo, ripoti za sasa zinadai kuwa Jose Mourinho ametupa karata yake ulingoni baada ya kujenga mahusiano ya karibu, pamoja na kwamba klabu ya Stamford Bridge kuonyesha nia, ila uhusiano na Red Devils uko wazi baada ya Ronaldo kueleza kwa hisia kuwa; “Naipenda Manchester.
“Kila mmoja analijua hilo – nimelizungumza mara nyingi. Manchester ipo moyoni mwangu. Nimewaacha marafiki wazuri pale, mashabiki wa ajabu na natamani kurudi siku moja.”
0 comments:
Post a Comment