Jaji wa kesi ya Oscar Pistorius ametupilia mbali hukumu ya mauaji ya kukusudia, na kusema mashtaka yalishindwa kuthibitisha kuwa (Oscar) alimuua mpenzi wake kwa kukusudia baada ya malumbano...>>>>
Ila Jaji Thokozile Masipa pia alikataa hoja za walalamikaji kwamba mwanariadha huyo alikosa uwezo wa kujizuia kufanya uhalifu.
Jaji alisema aliridhishwa na mshtakiwa “kuweza kutofautisha kati ya baya na zuri,” alisema alikuwa shuhuda aliyejaribu kuepuka ila haimanishi alikuwa mkosaji.
Mwanariadha huyo wa Olimpiki wa Afrika Kusini anakataa kumuua Bi Steenkamp siku ya Valentine mwaka uliopita, akisema alifikiri ni jambazi.
Oscar Pistorius atakabiliwa na hukumu ya kifungo cha muda mrefu jela endapo Jaji atamkuta na kosa la kuua kwa bahati mbaya.
0 comments:
Post a Comment