Hii ni moja ya stori kubwa za Magazeti ya leo Tanzania ambapo gazeti la Uhuru limeandika kwamba Rais wa shirikisho la muziki Tanzania Addo Novemba amefutwa kazi baada ya kuhusika na upotevu wa pesa za rambirambi ya Mwanamuziki...>>>>
Zilikua ni pesa zilizotolewa kama rambirambi kwenye msiba wa Mwanamuziki wa siku nyingi Tanzania mzee Gurumo ambazo zilikua ni milioni 1.1.
Fedha hizo zilikua zitumike kumnunulia Bajaji mke wa Marehemu Pili Kitwana lakini ikashindikana ambapo sasa nafasi hiyo ya Rais inashikiliwa na Stara Thomas kwa muda.
Addo Novemba alivuliwa madaraka hayo mwezi uliopita lakini alipinga uamuzi huo akidai ni batili lakini sasa Katibu wa shirikisho hilo amesema Wanachama wameridhia kumng’oa kwa sababu ameichafua TMA.
0 comments:
Post a Comment