‘Nimefuata maslahi Azam’ Amri Kiemba


Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Amri Kiemba amesema amekwenda Azam kufuata maslahi.
Kiemba alimwambia Mwandishi Wetu kuwa anaamini maisha popote, licha ya kukumbana na changamoto kadhaa......
Nyota huyo alisema ataitumikia Azam kwa juhudi zote iweze kutetea ubingwa wa Tanzania bara.
“Changamoto zipo, nivumilia mambo mengi Simba. Nimewahi kutuhumiwa kuhujumu, mara kiwango kimeshuka kwa sababu ya umri mkubwa. Yote nimekuwa na uvumilivu nayo,” alisema Kiemba.
Alisema anaamini kila mchezaji anataka maslahi, hivyo hakuona sababu ya kuacha kuichangamkia fursa ya kusajiliwa Azam FC.
Aliwataka mashabiki wa Azam kumpa ushirikiano ili kuiwezesha Azam kupata mafanikio katika michuano ya Ligi Kuu na michuano ya Klabu Bingwa mwakani.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks