Earl Lloyd: Mmarekani mweusi wa kwanza kucheza NBA, afariki dunia


Earl Llyod alikuwa Mmarekani mweusi wa kwanza kucheza NBA
Earl Llyod alikuwa Mmarekani mweusi wa kwanza kucheza NBA
Earl Lloyd, Mmarekani mweusi wa kwanza kucheza Ligi ya Kikapu Marekani amefariki akiwa na miaka 86, AFP imeripoti.
Marafiki wa familia ya Lloyd walikiita kituo cha televisheni cha WXYZ cha mjini Detroit kuripoti kifo cha Lloyd ambacho baadae kilithibitisha na chuo chake, Chuo kikuu cha Virginia Magharibi.
Lloys alionekana kwa mara ya kwanza NBA akiwa na timu ya Washington Capitols Oktoba 31, 1950.
Earl Lloyd akiwa na Detroit Pistons
Earl Lloyd akiwa na Detroit Pistons
Wachezaji wengine weusi wa Marekani Charles Cooper wa Celtics na Nat Clifton wa Knick wote waliingia NBA katika msimu 1950-51.
Lakini ratiba ya ligi ndio ilimfanya kuwa mweusi wa kwanza kucheza ligi hiyo, Lloyd alipewa jina la utani la “The Big Cat”.
Capitols walishindwa kujiendesha mwaka 1951, lakini Lloyd aliendelea na kushinda ubingwa mwaka 1955 akiwa na Syracuse Nationals na kumaliza miaka 10 ya maisha yake mchezo huo akiwa na Detroit Pistons.
Wakati wa kustaafu Lloyd alikuwa wa 43 kwenye orodha ya wafungaji wa NBA akiwa na alama 4,682. Alikuwa kocha wa Pistons mwaka 1971/72, na alikuwa Naismith Hall of Fame mwaka 2003
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks