JK ateua wabunge wawili wapya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.
Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.
Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.
Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
  • Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
  • Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
  • Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
  • Mhe. Janet Zebedayo Mbene
  • Mhe. Saada Salum Mkuya
  • Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
  • Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
  • Mhe. James Fransis Mbatia
Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidiz
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks