Michel Platini achaguliwa tena urais UEFA

Michel Platini amechaguliwa kuwa rais wa Uefa kwa mara ya tatu
Michel Platini amechaguliwa kuwa rais wa Uefa kwa mara ya tatu
Michel Platini alichaguliwa tena bila kupingwa kwa muhula wa tatu kaka rais wa UEFA kwenye kongresi ya mwaka Jumanne, na kudai chombo hicho kinachotawala soka Ulaya ni bora.
Sepp Blatter aliwekwa kitimoto kama mgeni na alipaswa kuvumilia kukosolewa kutoka kwa wapinzani wake wanaowania nafasi ya urais FIFA ambao walitakuwa kufanya uwasilishi wao kwa wajumbe.
Kwa njia nyingi, siku hiyo ilionyesha tofauti katika bodi hiyo inayoongoza soka Ulaya na ile ya dunia.
Wakati UEFA ikipata mafanikio ya kifedha ya Ligi ya Mabingwa, FIFA imekuwa ikikumbwa na mlolongo wa skandali za rushwa miaka michache iliyopita.
“Sisi ni wawazi, tuna demokrasia na bora,” Platini aliwaambia waandishi maripota.
UEFA imesema haitomuunga mkono Blatter atakapowania muhula wa tano May 29, ambapo anakabaliwa na upinzani kutoka kwa Luis Figo, Michael van Praag na Prince Ali Bin Ali Hussein.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks