Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa kiungo wake wa kati Jack Wilshere hauzwi, hiyo imekuja baada ya kuona matajiri wa jiji la manchester wanamnyatia kwa karibu.
Imeonekana kwa siku za hivi karibuni Manchester city inawahitaji wachezaji wenye vipaji ambao ni raia wa Uingereza.
Mchezaji mwingine anayewindwa na matajiri hao ni nahodha msaidizi wa klabu ya Liverpool Jordan Henderson ambaye ameonekana kuwa na kiwango kizuri msimu huu.
Hata hivyo Arsene Wenger ameongeza kuwa ana haraka ya kumuuza mchezaji yeyote ambaye ni zao la academy yake.

0 comments:
Post a Comment