Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Bibi Hillary Clinton ametangaza nia yake ya kugombea urais wa Marekani kwa kupitia chama chake cha Democrat mwaka 2016 na kuahidi kulinda maslahi ya familia za kawaida za Marekani.
Kwenye video iliyotolewa kwenye tovuti, Bibi Clinton amesema ingawa uchumi wa Marekani umefufuka kutoka kipindi kigumu bado unawanufaisha zaidi watu wenye uwezo. Ameongeza kuwa wamarekani wanahitaji mlinzi na yeye anataka kuwa mlinzi wao.
Bibi Clinton ana umri wa miaka 67 na ni mke wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na endapo atashinda kiti hicho atakuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo.
Je mama huyu ataweza kuongoza taifa ili kubwa duniani????????? toa mawazo yako.
0 comments:
Post a Comment