Mshambuliaji wa timu ya Chelsea Didier Drogba amezindua hospitali ya kwanza na kubwa kati ya tano alizoziahidi kuzijenga kama sehemu ya kujitolea kwa jamii yake.
Hospitali hiyo iliyopo wilaya ya Attécoubé katika mji wa kibiashara wa Abidjan, imemgharimu kiasi cha dola milioni moja za kimarekani na hospitali hiyo ni maalumu kwa wanawake na watoto wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Hospitali nyingine nne zilizobakia ziko katika hatua ya mwisho ya ujenzi kwenye miji ya Yamoussoukro, San Pedro, Man na Korhogo na zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao.
Hizi ni picha za hospitali hiyo:
Je kuna mchezaji yeyote Tanzania ambaye ameweza kusaidia hata jamii inayomzunguka kama yupo weka jina lake
0 comments:
Post a Comment