LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 14

Jimmy Baxter
HUSSEIN Ahmed Salah ni mwanariadha wa zamani(mbio ndefu) kutoka Djibouti akiweka rekodi ya kutwaa medali ya shaba katika michuano ya Olimpiki mwaka 1988. Kubwa zaidi ni pale aliposhinda kwa mara ya kwanza Michuano ya Dunia ya IAAF akitumia saa 2:08.09 mjini Hiroshima nchini Japan.

1995: India yaichapa Sri Lanka
KATIKA michuano ya kriketi barani Asia, India na Sri Lanka zilifika fainali baada ya kuzitoa Bangladesh na Pakistan mjini Sharjah, Falme za Kiarabu. Kukishuhudia India ikitwaa taji la nne la michuano hiyo. Mohammad Azhanurddin aliibuka ‘man of the match’ katika fainali hiyo.

2001: Baxter afariki dunia
JIMMY Baxter ni mwanasoka wa zamani wa klabu ya Rangers ya Scotland na Nottingham Forest ya England. Alizaliwa Hill of Beath huko Uskochi Septemba 29, 1939 na kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 61 jijini Glasgow. Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson aliwahi kusema kuwa Baxter alikuwa mchezaji bora katika soka la Scotland hakuna mfano wake.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks