LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 15



1984: Tommy Cooper afariki dunia
THOMAS Fredrick Cooper alikuwa mchekeshaji na mwanamazingaombwe kutoka nchini Uingereza ambaye alipoteza maisha akiwa na umri wa miaka 62, wakati akifanya kipindi cha moja kwa moja “live” katika runinga ya taifa. Sababu za kifo chake ni ugonjwa wa moyo. Alizaliwa Machi 19, 1921 katika kitongoji cha Caerphilly-Glamorgan, Wales. Alianza kuwika mwaka 1948. Mkali huyo alizikwa katika makaburi ya Mortlake. 

1989: Mashabiki 96 wa Liverpool wafariki dunia
KATIKA mtanange wa nusu fainali ya Kombe la FA, kwenye uwanja wa Hillsborough, Sheffield nchini England, kati ya Liverpool na Nottingham Forest; ukuta uliporomoka na kuua mashabiki 96 na 766 kujeruhiwa, siku hiyo Steven Gerrard akiwa na miaka 10 hakwenda kutazama mtanange huo. Uwanja huo unabaki kuwa miongoni mwa viwanja vilivyosababisha majanga makubwa katika ulimwenguni wa soka.

2013: LeParmentier afariki dunia
AKIWA na umri wa miaka 66, mwigizaji kutoka Marekani aliyekuwa akiishi England, Richard LeParmentier alipoteza maisha ghafla katika mji wa Austin, Texas nchini Marekani alikokwenda kuitembelea familia yake. Alifahamika sana katika filamu ya “Star Wars Episode IV: A New Hope (1977)” akitumia jina  la  Admiral Motti. Pia katika “Who Framed Roger Rabbit (1988)” akitumia jina la Luteni Santino. Alizaliwa Julai 16, 1946 mjini Pittsburgh, Pennsylvania.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks