Wakati ligi kuu ya Uingereza ikielekea mwishoni wachezaji wa Arsenal wameonekana kurudi kwenye viwango vyao baada ya kushinda mechi nane mfululizo na kama wangeanza hivi katika mechi za mwanzoni tungekuwa tunawapigia mahesabu ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu lakini kwa kipindi hiki tunawapigia mahesabu ya kushika nafasi nne za juu.
Lakini kwasasa klabu hiyo ina mpango wa kuwatema baadhi ya wachezaji na kuleta wachezaji wapya mwishoni mwa msimu huu na wachezaji watano ambao wametajwa kutemwa msimu ujao ni:
Abou Diaby
Mchezaji huyu amekuwa akikosa nafasi kwenye kikosi cha Arsene Wenger kutokana na kiwango chake kuwa chini ukilinganisha na wachezaji ambao wanaunda kikosi cha kwanza cha washika mtutu hao.
Per Mertesacker
Mjerumani huyu amekuwa akilahumiwa kwa kufanya makosa ambayo yanaigharimu timu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika mbio zake za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza.
Wojciech Szczesny
Kwa kipindi kirefu mlinda mlango huyu alikuwa ni mmojawapo wa mashujaa ndani ya kikosi cha Arsene Wenger lakini kiwango chake kilishuka ghafla na nafasi yake kuchukuliwa na raia wa Colombia Ospina ambaye ameonesha umahiri mkubwa wa kulinda lango.
Thomas Rosicky
Msimu huu kiungo huyu amekuwa akikumbwa na majeraha ambayo yamemsababisha kushindwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha Arsenal.
Lukas Podolski
Mchezaji huyu alipelekwa kwenye kikosi cha Inter Milan kwa mkopo na kuna uwezekano mkubwa wa kutorudi Arsenal mwishoni mwa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment