Makamba: CCM, Ukawa wanachimbiana kaburi


Naibu waziri wa sayansi na teknolojia, Mhe. January Makamba
Naibu waziri wa sayansi na teknolojia, Mhe. January Makamba
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (pichani), amesema vyama vya siasa vya CCM na vunavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vinachimbiana kaburi na kusubiri mwingine kumzika mwenzake katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tawi la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) la Karume mjini hapa juzi, alisema uchaguzi mkuu wa mwaka huu vyama hivyo vimeandaliana kaburi na yeyote atakayemuwahi kumuua mwenzake atamzika.
“Uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu sana kwa CCM na Ukawa kutokana na wote kuchimbiana kaburi na kila atakayewahi atamfukia mwenzake na kukamilisha adhima ya kuingia Ikulu,’ alisema Makamba.
Aidha, Makamba alisema tabia ya wanasiasa kupita kuomba kura vyuoni, misikitini na makanisani, inaonyesha nia mbaya ya kutaka madaraka kwa namna hiyo.
Alisema baadhi ya makada wamekuwa wakizunguka katika taasisi za dini, kwa waendesha bodaboda na machinga ili kuwarubuni waweze kutoa matamko ya kuwa wanafaa kuongoza nchi.
Alisema joto la kisiasa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, limekuwa kubwa kwa CCM na Ukawa kabla ya hata muda wa kufanya kampeni haujaanza.
Aidha, Makamba alisema anapingana na baadhi ya watu wanaodai kuwa vijana hawafai kukabidhiwa madaraka makubwa ya kuongoza nchi.
“Nashangaa kuona vijana wengi wanakatishwa tamaa kuwa hawawezi kuwania nafasi nyeti, dhana hiyo ni mbaya sana na haipaswi kuendelea kuwapo,” alisema.
Makamba ni mmoja wa makada wa CCM waliotangaza kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais uchaguzi mkuu ujao.
Chanzo: NIPASHE

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks