Akon Thiam
|
1947: Abdul-Jabbar alizaliwa
JINA lake halisi ni Ferdinand Lewis Alcindor Jr. mzaliwa wa jiji la New York, Marekani akiwa mtoto pekee wa Cora Lilian. Huyu ni mchezaji wa zamani wa kikapu na kocha nchini humo akiweka rekodi ya kucheza misimu 20 ya NBA katika klabu za Milwaukee Bucks na Los Angeles Lakers. Pia aliweka rekodi ya kutwaa MVP wa NBA mara sita. Mwaka 1996 alitunukiwa kuwemo katika orodha ya wachezaji mahiri 50 wa kikapu katika historia ya NBA.
1960: Rafa Benitez alizaliwa
RAFAEL BenÃtez Maudes ni kocha wa klabu ya SSC Napoli ya Italia, akiwika sana alipokuwa na klabu ya Liverpool na Chelsea. Alizaliwa jijini Madrid na kukulia katika akademi ya Real Madrid. Akiwa na umri wa miaka 26 alikuwa katika benchi la makocha wa Los Blancos na kocha msaidizi wa timu ya wakubwa. Aidha alizinoa Real Valladolid na Osasuna licha ya kutopata mafanikio.
1973: Akon alizaliwa
MWANAMUZIKI wa R&B na Hip Hop kutoka nchini Marekani Akon Thiam alizaliwa St. Louis katika jimbo la Missouri, Marekani. Katika maisha yake ya utoto aliishi nchini Senegal akiwa na wazazi wake waliokuwa wanamuziki. Alijifunza vyombo vitano vya muziki ikiwemo ngoma, gitaa na djembe. Akiwa chini ya udhamini waKonvicted alitwaa tuzo tatu za Grammy.
0 comments:
Post a Comment