LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 17



Victoria Beckham
1974: Victoria Beckham azaliwa
VICTORIA Beckham ni mfanyabiashara, mwimbaji  na mwanamitindo kutoka nchini Uingereza. Ana mume msakata kabumbu wa zamani wa timu ya taifa ya England David Beckham waliyeoana naye mwaka 1999. Mkali huyu alianza kuwika miaka ya 1990. Alizaliwa katika Hospitali ya Princess Alexandra mjini Harlow mashariki mwa London katika jimbo la Essex. Alifahamika zaidi akiwa na kundi la muziki wa pop la Spice Girls.

1983: Andrea Marcato azaliwa
ANDREA Marcato ni mchezaji wa rugby wa Italia na klabu ya Calvisano. Alizaliwa kaskazini mwa Italia katika mji wa Padua. Ameitumikia timu ya taifa ya rugby ya Italia akicheza mechi 16 na kuipa pointi 81 (2006-2010). Alisajiliwa na klabu ya Calvisano mwaka 2011 akicheza mechi 7 hadi sasa na kuipa pointi 46. Aliwika sana alipokuwa na vilabu vya Petraca na Benetton Treviso.

1998: McCartney afariki dunia
LINDA Louise ‘Lady McCartney’ Eastman alikuwa ni mwanamuziki, mpiga picha na mwanaharakati wa haki za wanyama kutoka Marekani. Alifahamika zaidi baada ya kuolewa na mwanamuziki wa kundi la The Beattles, Paul McCartney mwaka 1969. Walifunga ndoa katika Kanisa la St. John Wood. Mwaka 1995 alipatwa na kansa ya matiti hatimaye alipoteza maisha akiwa na umri wa miaka 56 mjini Tuscon, Arizona. Alizaliwa Septemba 24, 1941 jijini New York, katika viunga vya Scarsdale, Westchester County.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks