LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 18


KourtneyKardashian
SHIRIKA la Utangazaji la Uingereza (BBC) lilitoa tangazo kuwa hawatakuwa na taarifa ya habari siku hiyo. BBC ilianzishwa na John Reith ambaye alifariki Juni 16, 1971. Ilianza kurusha matangazo yake Oktoba 18, 1922. Makao makuu yapo Portland Place, jijini London.

1979: Kourtney Kardashian azaliwa
KOURTNEY Mary Kardashian ni Mmarekani, mwanamitindo na mahiri katika utangazaji vipindi vya runinga. Mkali huyu ana wadogo zake wa kike Kim na Khloe ambao wanafanya vizuri kama alivyo yeye. Alianza kuwika mwaka 2004. Alizaliwa Los Angeles, California. Makazi yake kwa sasa yapo Calabasas, California. Ana mume waliyefunga naye ndoa mwaka 2006, Scott Disick. Katika runinga ana vipindi vipi kikiwemo kile cha ‘Keeping Up with Kardashians’. Katika siku ya kuzaliwa Kourtney anaungana na wasakata kabumbu mlinda mlango wa Arsenal, Wojciech Sczczesny na Divorck Origi aliyetolewa kwa mkopo Lille akitokea Liverpool.

2014: Dylan Tombides afariki dunia
DYLAN James Tombides alikuwa msakata wa kabumbu wa klabu ya West Ham, England. Hadi mauti yanamkuta alikuwa na umri wa miaka 20. Alizaliwa Perth nchini Australia  Machi 8, 1994. Akianza soka lake katika timu ya U-17 ya West Ham. Kabla ya kutua hapo akiwa Australia alikuwa na klabu ya Stirling Lions na Hong Kong. Alifariki kwa kansa ya kizazi alipewa jezi namba 38 ambayo imepumzishwa kama ilivyokuwa kwa Bobby Moore.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks