LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 19

Maria Sharapova
CHARLES Joseph John ‘Joe’ Hart ni mlinda mlango wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya England. Leo katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwake anaungana na msakata kabumbu wa zamani wa Brazil, Rivaldo (1972). Joe Hart alizaliwa Shrewsbury Town. Soka lake lilianza katika klabu ya Shrewsbury Town mwaka 2003-2006. Manchester City ilimsajili mwaka 2006 hadi sasa. Mwaka 2007 hadi 2010 Hart amekuwa kwa mkopo katika klabu ya Tranmere Rovers, Blackpool na Birmingham City.

1987: Maria Sharapova azaliwa
MARIA Yuyevna Saharapova ni mchezaji wa tenisi kutoka Russia ambaye Oktoba 2, 2014 aliwekwa katika orodha ya nyota wa pili kwa ubora duniani inayotolewa na WTA. Alizaliwa Nyagan wakikimbia madhara ya nyuklia mwaka 1986 katika mji wa Gomel, wakati mama yake Yuri akiwa na ujauzito wa Maria.

1989: Gazeti la The Sun laibua mkanganyiko
GAZETI la udaku linaloongoza kwa kusomwa kwa sasa hapa ulimwenguni la ‘The Sun’ lilisababisha mkanganyiko mkubwa, lilipoandika kuwa watazamaji waliokuwa katika tukio la Hillsborough wakati wa mtanange wa FA kati Liverpool na Nottingham Forest; walikuwa wakipora pesa katika maiti zilizotapakaa uwanjani hapo na majeruhi. Tukio la Hillsborough lilitokea Aprili 15, 1989 na kuua mashabiki 96 na 766 kujeruhiwa. Gazeti la ‘The Sun’ lilianzishwa mwaka 1964 sasa lipo chini ya Rupert Murdoch.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks