1984: Jenna Shoemaker azaliwa
Carly Rose Sonenclar
|
1999: Carly Rose azaliwa
CARLY Rose Sonenclar ni mwimbaji na mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Alizaliwa katika jiji la New York. Huimba nyimbo zake katika R&B, soul na pop. Alianza kuwika mwaka 2006 katika tamasha la ‘New York Music Theatre’ akiigiza kama Pearl katika ‘The Night of the Hunter’. Desemba 2012 alishika nafasi ya pili kwa msimu wa pili mfululizo wa X Factor.
2014: Rubin Carter afariki dunia
RUBIN ‘Hurricane’ Carter alikuwa bondia kutoka Marekani. Alizaliwa Juni 6, 1937 Clifton, New Jersey Alifariki Toronto nchini Canada akiwa na umri wa miaka 76. Alikuwa akijulikana ‘Hurricane’ kwa maana ya kimbunga anapokuwepo ulingoni. Alitupwa jela kimakosa baada ya kupatikana na makosa ya kuua, na kuachiwa baada ya miaka 20 ya kukaa lupango.
0 comments:
Post a Comment