LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 21




1926: Queen Elizabeth II azaliwa

Queen Elizabeth II
MALKIA Elizabeth II ni miongoni mwa wajumbe 16 kati ya 53 wa Jumuiya ya Madola. Alizaliwa Mayfair jijini London, England. Jina lake halisi ni Elizabeth Alexandra Mary. Alianza kutawala Uingereza tangu Februari 6, 1952 mpaka sasa. Anatimiza miaka 89 tangu kuzaliwa kwake katika taifa hilo ambalo King Henry VI aliruhusu soka lianze kuchezwa baada ya waraka wa Mfalme Edward II kupitia kwa Meya wa Jiji la London mwaka 1314 kutoruhusu mchezo huo kuchezwa katika ardhi hiyo.

1960: Brasilia yazinduliwa
BRASILIA ni mji mkuu wa Brazil ambako taifa hilo limejipatia umaarufu mkubwa kutokana na wachezaji wa soka wengi kupatikana kutoka huko. Itakumbukwa kwamba tangu mwaka 1763 -1960 mji mkuu ulikuwa Rio de Janeiro. Mwaka 2014 jiji hilo la nne kwa idadi kubwa ya watu nchini humo, lilipewa hadhi ya kutayarisha michuano ya Kombe la Dunia, awali mwaka 2013 liliandaa Michuano ya Mabara.

1992: Isco azaliwa
FRANCISCO Román Alarcón Suárez maarufu kwa jina la Isco ni mwanasoka wa Hispania anayeitumikia klabu ya Real Madrid katika nafasi ya kiungo mshambuliaji. Alizaliwa mjini Valencia ambako alianza kuitumikia klabu ya Valencia kabla hajajiunga na Málaga CF mwaka 2011. Pia ameitwa kwenye timu ya taifa tangu mwaka 2008.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks