Ndege ya jeshi nchini Algeria imeanguka ikiwa imebeba zaidi ya watu 100.



Redio ya taifa inasema ndege hiyo aina ya Hercules C-130 ilianguka katika eneo la milima katika jimbo la Oum El Bouaghi kusini mashariki mwa mji mkuu , Algiers na ilikuwa imewabeba abiria 103 wakiwemo wafanyakazi wa ndege.

Kuna taarifa kwamba ndege hiyo ilikuwa imebeba wanajeshi na jamaa zao waliokuwa wakisafiri kuelekea jiji la Constatine.
Miili 71 ya watoto na wanawake imepatikana katika eneo la ajali
Taarifa zinasema kuwa wamepata mtu mmoja aliyenusurika huku waokozi wakiendelea kutafuta manusura zaidi.
Duru zinasema kuwa upepo mkali pamoja na hali mbaya ya anga ndiyo huenda ilisababisha ndege hiyo kuanguka.
Jeshi halijatoa taarifa yoyote mpaka sasa.
Ajali hii inasemekana kuwa mbaya zaidi kushuhudiwa katika mwongo mmoja na ya tatu ikihusisha ndege ya jeshi.
Ndege nyingine ya kampuni ya Air Algerie Boeing 737, ilianguka punde baada ya kuruka kutoka mjini Tamanrasset mnamo mwaka 2003,na mtu mmoja pekee ndiye alinusurika
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks