Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook wameanzisha kampeni kubwa kuitaka kampuni hiyo kuondoa picha za binti mdogo mwindaji anayeonekana amepiga picha na wanyama wakali anaodai kuwaua katika nchi za kiafrika ikiwemo Zimbabwe...>>
Binti huyo Kendall Jones kutoka Cleburne, Texas, anadaiwa kuwa ni mwindaji mdogo zaidi kuwapiga risasi wanyama hao wakali wa mwituni akiwemo Chui na kuthibitisha hilo amekuwa akipozi nao kwa picha baada ya kufanya kitendo hicho.
Maelfu ya watu wanaitaka Facebook kuondoa picha hizo ambapo binti huyo amejitetea kuwa anafurahi kuendeleza ndoto zake.

Binti huyo amekuwa akitabasamu na kuweka pozi pembeni ya wanyama wa aina mbalimbali anaodai kuwaua ambapo picha hizo zimeamsha hisia kali katika mitandao ya kijamii watu wakidai ziondolewa.
0 comments:
Post a Comment